Hakuna mvua ya kutosha: Idara ya utabiri wa hali ya hewa yashauri wakulima Kwale kukaza kamba 

Na Jumwa Mwandoro

Idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kaunti ya Kwale imewataka wakulima kutafuta ushauri Kwa idara ya kilimo kuhusu aina ya mimea watakayo panda ili kuepuka kukabiliwa na uhaba wa chakula.

Agizo hilo ni kutokana na ukosefu wa mvua za kuridhisha katika msimu huu wa mvua fupi za mwezi wa Octoba na Novemba.

Kulingana na mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kaunti ya Kwale Danson Ireri, mara nyingi kaunti hiyo hushuhudia mvua chache lakini msimu huu hali imekua mbaya.

Ireri amesema kuwa msimu huu wamerekodi mvua kidogo ya asilimia 30.

Mimea ya kunde shambani katika eneo la Mbuwani, Kwale

“Nawasihi wakulima kuchukua hatua mapema na kutafuta ushauri kwa idara ya kilimo ili kufahamu aina ya mimea inayotoa mazao haraka na kwa mda mfupi .” Ireei alisema.

Wakati uo huo amewataka walio na uwezo wa kuvuna maji ya mvua kufanya hivyo ili kuyatumia katika shuguli za kilimo cha unyunjizaji.

Ameongeza kua wakaazi wachukue mfumo wa kujibunia mashamba ya bustani nyumbani kwao ili kujipatia baadhi ya bidhaa kwa ukaribu na kuimarisha lishe.

“Ni wakati sasa wakaazi wachukue mfumo wA kilimo cha unyunyiziaji badala ya kusubiri mvua chache ambazo zinanyesha kwa kasi ndogo na badala yake. Hii itawasaidia w kujipatia chakula bila tatizo lolote,” alisema Ireri.

Scroll to Top