Na Jumwa Mwandoro
Idara ya usalama katika kaunti ya kwale imeelezea kutoridhishwa kwake na visa vya dhuluma za kijinsia dhidi watoto.
Ii ni baada ya visa 123 kuripotiwa mwaka huu 60 kati ya visa hivyo vikiwa vya eneo la Msambweni pekee,
Kulingana na kamanda wa polisi wa kwale Ali Nuno, takwimu hizi ni za kuvunja moyo na hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa.
“Kulingana na twakwimu tulizo nakili kuanzia mwaka 2022 visa hivi vimekua vya kuongezeka kila uchao hali inayotia waswasi,” alisema Nuno.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nyumba salama ya watoto na kina mama waliopitia dhuluma mbalimbali huko Msambweni, Nuno amesema ipo haja ya asasi za usalama kuja pamoja na kulizungumzia kwa kina swala hili ili kutafuta suluhu ya kudumu.

Nuno amesema ni jambo la kusikitisha kuona visa hivi vinatokea katika Jamii zetu bila mikakati kabambe kuchukuliwa kuhakikisha vinakomeshwa.
Wakati huohuo ameeleza kuwa wameweka vifaa muhimu katika jengo la watoto katika kituo cha polisi cha Diani kama njia ya kukabiliana na maswala hayo ya kikakatili.
“Tuko na nafasi ya kutosha na yenye vifaa hasa kwa watoto waliopitia dhuluma kwa hivyo wale wanaohusika na kuokoa watoto basi wanaruhusa ya kuwapeleka watoto wakati taratibu za kutafuta haki zikiwa zinaendelza,” Nuno alisema.
Kwa upande wake hakimu wa mahakama ya Msambweni Leah Kabaria amesema kuwa sote tunajukumu katika kuwalea watoto ili wapate malezi mema.
Leah ameeleza kuwa siku hizi watoto ndio wanaongoza katika visa vya dhuluma dhiririsho kuwa hawapati malezi bora.
“Tuna wajibu wakuwaeleza watoto wetu mambo waziwazi na kwamba utumizi wa utandawazi usipodhibithiwa hasa kwa watoto basi tunaelekea pabaya,” alisema Leah

Leah alsima jamii pia inajukumu kuripoti visa hivi na sio tu kumaliza kesi zao kinyumbani au kuficha ushahudi pale unapotakikana.
“Mara nyingi tumepata changamoto pale tunapotafuta ushahidi kwani wengi umelizia kesi zao kinyumbani au hata kutoroshwa hivyoo kuifanya safari ya kutafuta Haki kuwumbwa na changamoto,” alieleza Leah.
Nae afisa katika shirika la International justice commission Naomi Maina, amezitaka Jamii kutekeleza majukumu yao ya ulezi ipasavyo ili kuepuka visa kama hivi kutokea.
“Pale mzazi mmoja anapochukua uamuzi wa kwenda ugaibuni kutafuta ajira basi ni dhiririsho kuwa muongozo wa familia husika niwakutiliwa shaka, ni jukumu letu kuhakikisha tunawakuza watoto wetu Kwa misingi bora,” alisema Naomi.

Alisema mtoto anapokuzwa katika mazingira ya kirafiki basi atakua akiwa mwema na mwenye heshima nzuri.
Aliongeza kuwa kunahitjika ushirikiano kati ya idara ya usalama na washikadau mbalimbali ili kujatafuta suluhu ya jimsi ya kukinga kizazi cha sasa.
“Siku hizi ni aibu kuona hata mtoto wa kiume anabakwa jambo linaloonyesha kuwa tumewacha mila na tamaduni ambazo zilikua na muungozo mwema,” alieleza Naomi.
Washika dau adiha ameongeza kuwa kuna haja ya hamasa zakutosha kupeanwa kwa jamii ili kupunguza visa hivyo.













