Na Bintkhamis Kadide
Kutelekezwa kwa mmea wa mnazi Pwani kumepelekea waekezaji wengi kubadili nia ya kuweka viwanda katika kaunti za pwani kufuatia idadi ndogo ya minazi iliopo.
Haya ni kwa mujibu wa na msimamizi wa kituo cha utafiti wa kilimo na mifugo (KALRO) eneo la Matuga Finyange Pole.
Pole amesema kuwazoezi la kuhesabu mimea lililofanywa mwaka wa 2020 lilionyesha pwani nzima kwa jumla ina idadi ya minazi milioni 10 jambo alilolitaja kudharaulika kwa mmea huo ikizingatiwa kwamba mnazi unafaida nyingi kwa mkulima na jamii nzima.
Akizungumza huko Matuga Pole amesema kuwa kwa muda mrefu mmea wa mnazi umehusishwa na mabo ambavo hayana thamani kufuatia kupatikana pombe ya mnazi hivyo kushushwa hadhi yake.
Aidha ameendelea kueleza kuwa kando na faida ambazo mkulima hupata kupitia mmea huo kuna changamoto ya kiangazi sawia na kuvamiwa na wadudu wanaoathiri mazao ya mnazi ambapo mabadiliko tabia-nchi ni sababu kuu.
Pole amewataka viongozi katika jumuiya ya kaunti za pwani kuja na mbinu ya kuboresha kilimo cha mmea wa mnazi na pia kupanda minazi mingine kwani iliyopo ni ya kitambo mno hivyo haina mazao mazuri.












