Na Caroline katana
Shirika la kimataifa la uhamiaji wa binadamu (IOM) limeungana na mamlaka ya ajira nchini (NEA) kutengeza kitabu cha mwongozo kitakachotoa maelezo kamili kuhusu mataifa tofauti tofauti ambayo vijana wanaenda kutafuta ajira.
Kitabu hicho kitafahamika kama “Pre Departure Information Handbook”.
Hii ni baada ya asilimia kubwa ya vijana wanaoenda ngambo kufanya kazi kukosa kufahamu sheria za mataifa hayo pamoja afisi za mabalozi wa Kenya wanaohudumu katika mataifa hayo, jambo linayowapa changamoto ya usaidizi wakati wanapokumbana na matatizo.
“IOM pia inashirikiana na serikali kutengeza sera za mfumo wa uhamiaji wa wafanyikazi ambazo vijana wanaezasafiri nazo ili ziwape mwongozo wa utendakazi. Ni sharti vijana wawe na ufahamu wakutosha kuhusu nchi wanazoenda ili waweze kuwa na urahisi wa kuripoti masaibu watakayowakumba,” alisema aAfisa wa shirika la IOM Roy Odhiambo.
Odhiambo aliongeza kuwa serikali ya Kenya imeingia katika makubaliano ya uhamiaji wa kazi baina ya mataifa 6 yakiwemo Ujerumani, Saudi Arabia, Qatar, Uingereza, Austria na Canada huku mikakati ya maelewano na taifa la Kuwait ikiendelea.
“Taifa la Kenya linashuhudia idadi kubwa ya vijana wanaokosa ajira ambapo sasa serikali inatafuta nafasi ya vijana kuapata ajira huko ng’ambo kwa sababu uchumi wa Kenya hauezi ajiri kila mtu, tunaona hatua yenye serikali imechukua ili kuwasaidia vijana na soko letu linazidi kuongezeka kwani mazungumzo na taifa la Kuwait yanaendelea,” alisema.Odhiambo.
Odhiambo alisisitiza kuwa jukumu kuu la shirika hilo ni kukuza uhamiaji salama na wa kawaida katika kuangazia haki na ustawi wa wasafiri wanaofanya kazi katika mataifa ya nje.

Mwenyekiti wa CSO Migrant Network, Alfred Sigo
“IOM imeshirikiana na mamlaka ya kitaifa ya ajira pamoja na mshirika ya kijamii ya kutetea haki za wahamiaji kufanya kampeni ya kuwahamasisha vijana eneo hili la Likoni kuhusu njia salama za usafiri ikiwemo stakabadhi hitajika na ma ajenti halali waliosajiliwa na NEA,ili watume maombi ya ajira za nje kupitia tovuti ya NEA. Hii itawasaidia kuepuka dhulma kutoka kwa ma ajenti feki pamoja na kuhakikisha usajili unaozingatia haki za uhamiaji w kwa wafanyikazi katika afisi husika,” aliongeza Odhiambo..
Hata hivyo anasema kuwa wanajenga uwezo mashirika ya kijamii ya kutetea haki za wahamiaji ili waweze kuwa mabalozi wa kukuza na kulinda haki za wafanyikazi wahamiaji.
Mwenyekiti wa CSO Migrant Network eneo la Pwani ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa shirika la Pwani Youth Alfred Sigo ameafiki awali kuwepo na kesi nyingi za vijana na akinamama. kulaghaiwa na ma ajenti feki.
“Kabla ya kuanzishwa kwa kampeni za hamasa, vijana na akinamama waliotaka kusafiri walikuwa wakidhulumiwa fedha zao ,lakini kwa sasa hivi kesi hizo zimepungua kwani watu wengi wanatuma maombi ya kazi kupitia lango la NEA,” aliema Sigo.
Sigo alitoa changamoto kwa vijana kuwa wabunifu ili kutengeza nafasi za ajira binafsi zitakazofungua ajira kwa vijana wengine.
“Vijana wanapojitengezea ajira na kuajiri wengine, inapunguza mzigo wa ukosefu wa ajira nchini,” alisema Sigo.
Aliongeza kuwa hamasa hio imeweza kuwafikia zaidi ya vijana elfu tano ukanda wa pwani.
“Nawasihi vijana waliopokea mafunzo haya pia waweze kueneza injili hii mashinani na hata wao wenyewe wachukulie mafunzo haya na umuhimu ili wanaotaka kusafiri wapate wepesi wa kutuma maombi ya kupata ajira ng’ambo,”alisema.

Mtetezi wa haki za wahamiaji Kwale, Halima Abbas
Halima Abbas ambayye ni mfanyikazi wa shirika Migrant Workers aliyesafiri katika mataifa matatu anaafiki kupitia changamoto kutoka kwa ajenti na waajiri wake.
“Nimewahi kusafiri katika taifa la Qatar, Misiri na Saudi Arabia, niliposafiri mara ya kwanza Saudi Arabia nilipata changamoto, mwajiri wangu alichukua pasipoti yangu akakaa nayo, ikawa hata kunipa nafasi ya kutuma pesa nyumbani ni shida, chakula pia ni shida, kunipa mshahara pia akawa hanipi, nikatafuta usaidizi kwa afisi ya leba nikarudi nyumbani lakini sikuvunjika moyo. Mara ya pili nikaenda Misiri, safari hii nilipata ajenti feki, nilipofika uwanja wa ndege nikawa sina kwa kuenda maana ajenti alikuwa hashiki simu zangu, nikatafuta usaidizi kwa watu wa leba kwa mara nyengine nikarudi nyumbani,” alielezai Halima.
Halima akisema kuwa changamoto za kimaisha zilimchochea pakubwa kusafiri mataifa ya nje kwa matumaini ya kupata fedha za kukimu mahitaji ya familia yake.
“Niliachika na nina watoto wanahitaji kusoma nan chi yetu ya Kenya inakumbwa na uhaba wa ajira ,kwa hio nikawa na matumaini ya kupata pesa nikiwa Ughaibuni ,lakini nilipata changamoto ndipo nikarudi nyumbani na hadi kufikia sasa mimi ni balozi wa kutetea haki za wahamiaji,” alisema.
Baadhi ya wakenya wanaotafuta ajira katika mataifa ya nje wakekuwa wakijipata katika njia panda kwa kukosa mwongozo wa kisheria za mataifa.












