Taharuki Diani kufuatia mauaji ya mwanaume wa miaka 29

Na Mwandishi Wetu

Mwanaume wa umri wa miaka 29 ameuawa alasiri ya leo kwa kudungwa kisu na watu wawili waliokua kwenye bodaboda.

Inadaiwa Juma Said alikua akielekea Msikitini kabla ya kukutana wawili hao walionza ugomvi naye kabla kumdunga.

Juma alikua mwendesha bodaboda katika eneo la Bongwe Gombato.

Mauaji hayo yalisababisha taharuki baada ya wakaazi kuzua rabsha na kutaka kuvamia kituo cha polisi cha Diani wakidai washukiwa hao waliotiwa mbaroni kutolewa ili wawapige,

Iliwalazimu maafaisa wa polisi kuingilia kati na kufyatua vitoza machozi kutuliza hali.

Kamanda wa Polisi wa Msambweni Ahmed Hillow amedhibitisha kisa hiho akisema wawili hao walimdunga kisu kwenye tumbo na baadaye akakimbizwa hosipitalini na kufariki akihudumiwa.

Hillow amesema wawili hao watazuiliwa katika kituo hicho Diani na watafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

ReplyForwardAdd reaction
Scroll to Top