Hali tete Diani, magenge ya vijana wadogo yazindisha uvamizi kwa mapanga

Na Mwandishi Wetu

Magenge ya vijana wadogo wameendeleza uvamizi ktika mji wa Diani kwa kukata wakaazi kwa mapanga na kuwadunga visu.

Vijana hao walihangaisha watu siku ya Jumamosi na kuufanya mji wa kitalii wa Diani kusalia katika hali ya taharuki.

Inadaiwa walichukua fursa ya mauaji yaliotekelezwa siku ya Ijumaa ya mwanaume wa miaka 29 wakisema wanafanya maandamano dhidi ya kisa hicho na kuwaibia wafanyi biashara na kuwapora wakaazi.

Mwandishi wa habari wa Msenangu FM Brivian Simiyu ni miongoni mwa walioshambuliwa siku ya Jumamosi.

Simiyu alikatwa kwenye sikio na kuporwa simu mchana peupe akielekea nyumbani.

“Nilikua nikitoka kazini mwendo wa saa nane hivi, nikiwa barabarani nilikutana na kikundi ya vijana kama sita hivi. Tukakaribiana nao kulikua na kijana mrefu akatoa panga nikajaribu kukimbia nikaakunda nikashtukia wamenikata sikio na wengine wananisearch wakaniibia simu” alsima Simiyu

Vijana hao pia walivamia biashara kadhaa kuiba bidha za elektroniki, vileo, pesa na simuza kazi.

Wafanyi biashara wengine walifunga maduka yao kufuatia taharuki hiyo.

Kamanda wa polisi eneo la Msambweni Ahmed Hillow amesema wameongeza doria katika mitaa yote ya Diani.

Scroll to Top