Na Jumwa Mwandoro
Mashirika saba ya kijamii kaunti ya kwale yameungana kuhamasisha jamii dhidi ya utunzaji mazingira sawia na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.
Hatua ii inajiri pale shuguli za ukataji miti kiholela umetajwa kuongezeka kwa kasi jambo linalopelekea kupungua kwa misitu katika baadhi ya sehemu.
kulingana na Mwenyekiti wa shirika la Tulinde future yetu initiative Salim Chiguza amesema kwamba mradi wao unalenga zaidi uhifadhi wa misitu akitaja kuwa misitu imekua ikitumika kama sehemu za kivutio Cha utalii hivyo ipo Kuna haja ya kulindwa.
”Tumejikita zaidi katika kuhamasisha jamii dhidi ya utunzaji mazingira kwani ukataji wa miti umepelekea kupotea kwa baadhi ya ndege ambao wamekua wakitumika kama kivutio Cha utalii hivyo tunataka kurudisha zile asili zilizokuwemo kwa misitu yetu.”alisema Chidzuga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Imara chini ya mwamvuli wa Sikiliza sauti Dunia Inaita uliodhaminiwa na shirika la We world uliojumuisha mashirika saba ya kwa lengo la kabiliana na mabadiliko tabia nchi.
Wakati huohuo ameeleza kuwa katika kampeni hiyo watatumia mbinu ya midahalo katika baadhi ya shule kama njia ya kuhifadhi mazingira wakiwa bado wangali wachanga.
” Tumechagua mbinu ya kuwajumuisha wanafunzi katika midahalo, ii itasaidia kuwajenga kiuwezo wakufahamu umuhimu umuhimu wa kuhifadhi mazingira wakiwa bado wachanga hivyo kubakia na ujumbe huo ambao ndio watakua mabalozi wa mazingira katika ukuaji wao.” alisema Chidzuga.

Kwa upande wake katibu wa Kaya kaunti ya kwale Hassan Randani amepongeza hatua hiyo huku akisema kwamba misitu imekua kama sehemu ya maisha yetu.
Randani amesema kwamba misitu imekua ikitumika kama dawa na vilevile sehemu za ibada hivyo Kuna haja zaidi ya jamii kuhakikisha wanaeneza ujumbe ili iweze kuhifadhi.
”Misitu imekua ikitumika kama dawa,mti wa mbuyu hasa umekua katika hatari yakupotea na wakati wetu tumeutumia kama sehemu ya kuabudu hivyo unafaa kulindwa, na ujumbe huu ni Bora zaidi ukienezwa kwa vizazi vichanga.” alisema Randani.
Nae afisa katika shirika la We world John Henny ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa mda wa miezi 8 Katika kaunti 3 nchini ikiwemo Kwale, Isiolo na Nairobi kwa lengo la kabiliana na mabadiliko tabia nchi.

John amesema kwamba kaunti ya kwale imebahatika kupata raslimani mbalimbali kama vile bahari na misitu hivyo ni jukumu la Mashirika kueneza ujumbe ili viumbe vinavyo tegemea sehemu hizi kupata uhifadhi Bora.
”Kupitia miradi hii kuna makundi yatakayo jikita zaidi katika kuhifadhi raslimani ya bahari kama vile mikoko hivyo viumbe vinavyo patika a kule kuwa katika mazingira Salama,” alisema John.
Mwisho












